Home || The Aggressive Vision || Prophetic Word Of The Lord || On Line Library || Current Articles and What's New
Free Literature || Visions from The Lord || More About ACMTC || Contact


Inamaanisha nini kuwa

Umeokolewa

(What it means to be

Saved)

WOKOVU WA KIBIBLIA ni mojawapo ya dhana kubwa kuliko zote zilizowahi kuingia katika fikra za mwanadamu. Neno “wokovu” linajumuisha yale yote ambayo Mungu anayofanya kutoka milele hadi milele, ya kumkomboa mwanadamu kutoka katika dhambi na madhara yake. WOKOVU NI KAZI YA MUNGU KWA MWANADAMU, NA NDANI YA MWANADAMU, SI MATENDO YA MWANADAMU, BALI MUNGU; INGAWAJE MTU ALIYEOKOLEWA KWELI HUFANYA KAZI KWA AJILI YA MUNGU! Tunaamini ya kwamba majadiliano haya yatapanua maarifa na kuridhika kwa msomaji kutokana na wokovu wa Mungu.

Wokovu hutoka kwa Mungu. Mungu Baba ndiye chanzo kikuu. Aliupenda ulimwengu kutoka milele zote, na akamtuma Mwanae aje kufa Msalabani, kwa ajili ya dhambi za ulimwengu. Mungu, Mwana, ni asili kuu ya wokovu kama vile Yesu Kristo, Mwana wa Mungu, ndiye aliyeleta wokovu wetu pale Msalabani katika kufufuka Kwake, na kwa huduma ya kimbingu. Chanzo cha uzima na wokovu wa mtu BINAFSI ni Mungu, Roho Mtakatifu ambaye hushuhudia, hutia nuru, hutuhuisha na kutuwezesha.

Asili ya wokovu iliyofunuliwa ni Maandiko. Ujumbe uliomo ndani yake uweza wa Mungu uletao wokovu, kwa kila aaminiye. (Rum. 1:16) na yakuwa tangu utoto umeyajua maandiko matakatifu, ambayo yanaweza kukuhekimisha hata upate wokovu ( 2 Tim. 3:15), na yana mambo yote muhimu kuhusu uzima wa milele. (Yoh 20:31; 1 Yoh 5:13).

     Agano Jipya linayo maneno mengi, aya nyingi na habari nyingi zinazo onyesha masuala mbalimbali ya wokovu. KUNA WOKOVU MMOJA TU, LAKINI MSAMIATI WAKE INATOFAUTIANA KATIKA VOKOVU KULINGANA NA KITU MUDA, WAKATI ULIOPITA, ULIOPO NA UJAO. Tunatamani kukiona kile ambacho Mungu alikifanya kwa ajili yetu, kabla hatujaamini, na kile alichotufanyia mara tu tulipoamini, na kile ambacho atatufanyia bado kwa sababu tumeamini.

    Agano Jipya linafunua kwamba Mungu alikuwa akitenda kazi kwa ajili yetu hata kabla hatujapata kumfikiria. Yeye ndiye chanzo cha wokovu wetu. Hebu tutafakari hili.

I. Kile Mungu alichotufanyia kabla hatuja amini:

A.  Alichowafanyia wanadamu wote kwa ujumla bila kujalisha kama wana amini au la.

1.    Aliwaumba

2.  Amewahifadhi na kuwatunza

3.   Aliwapa akili, hukumu na dhamiri

4.  Mpango wote wa wokovu ameufanya kuwa sheria

5.   Aliivuvia Biblia, akaitunza, na kwa mpangilio unafaa akafanya Biblia kuchapishwa na kusambazwa.

6.   Alimtuma Roho Mtakatifu duniani kwa ujumbe wa uinjilishaji (Yoh 16:8-11; 3:5).

7.  Aliwapenda (Yoh 3:16)

8.   Huita na kutuma wahubiri na wamisionari ili kupeleka ujumbe wa wokovu kwao.

9.   Katika Ulimwengu wa asili, aliweka ufunuo wa kutosha wa nguvu yake ya milele na hekima yake ya kuwadhihirishia wale wanaomtafuta kwa moyo wa dhati juu ya kuwepo kwake na pia Enzi yake (Rum. 1:19-20).

10. Huwavumilia sana wasio amini na kuwapatia muda wa kutosha na fursa za wao kuweza kuokolewa (2 Pet. 3:9; Rum. 2:4).

 

K.  Ni nini Mungu alichokifanya kwa waaminio kabla hawajaamini, tukiongezea na hayo:

1.  Aliwajua kwanza (Rum. 8:29, 1 Pet. 1:2).

2.  Aliwachagua (Efe. 1:4).

3.  Aliwakomboa, au aliwanunua (Ebr. 9:12).

4.  Aliwapatanisha (2 Kor. 5:18, 19; Rum. 5:10).

5.  Aliwapa Mwanae (Yoh 6:37; 17:6, 12).

6.  Aliwaita waliokataliwa (Rum. 8:30).

7.  Aliwashuhudia kwa habari ya dhambi, haki na hukumu (Yoh 16:8-11).

8.  Aliwavuta kwake (Yoh 6:44).

9.  Aliwajalia kuja kwa Kristo (Yoh 6:65).

10.Aliifungua mioyo yao (Mdo 16:14).

11.Aliwaongoza kwenye toba kwa wema wake (Rum. 2:4; Mdo 5:31).

12.Aliwapatia imani ya kuamini(Yoh 10:26; Mdo 13:48; Efe. 2:8, 9).

 

Rejea hizi zinafunua kile MUNGU alichokifanya katika kutuleta sisi mahali pa imani iokoayo. Sasa, tuko tayari kuangalia mbali zaidi.

 

II. Kile Mungu alicho tufanyia punde tu tulipoamini:

 

    MAELEZO HAYA ni maneno ya Agano Jipya kwa baraka za mwazo katika maisha ya Ukristo. Zinafunua nguvu kuu ya wokovu wa Mungu uliotukuka. Kwa vile ziko sawia haupo utaratibu wa kupanga matukio au mpangilio wa kimantiki.

 

1.  Alitusamehe (Efe. 17; Mdo 10:43).

2.  Alituokoa (Yoh 3:3-7) au alitukirimia uzaliwa mpya (Yoh 1:13).

3.   Ametuhuisha na kutufanya hai (Yoh5:25; Efe. 2:1).

4.  Ametustahilisha (Rum. 3:28; 5:1; Mdo13:38, 39).

5.  Ametutakasa kwa uhusiano wake na sisi (Ebr. 10:14; 1 Kor. 1:30).

6.  Ametukamilisha milele (Ebr. 10:14).

7.  Ametuosha na kutufanya safi (Ufu. 1:5; Tito 3:5).

8.  Ametubatiza kwa Roho katika katika mwili mmoja (1 Kor. 12:13).

9.  Ametupiga chapa kwa Roho wake (Efe. 1:13, 4:30).

10.Ametufanya kuwa hekalu la Roho Mtakatifu (1 Kor. 6:19).

11.Ametuleta kwenye muungano muhimu na Kristo. (Yoh 15:1-7).

12.Ametukomboa kutoka katika nguvu za giza na kutuingiza katika Ufalme wa Mwanae mpendwa (Kol. 1:13).

13.Alitufufua na kutufanya kuketi pamoja na Kristo katika ulimwengu wa roho (Efe. 2:6).

14.Alituokoa (Mdo 16:31; Yoh 10:9).

15.Alitufumbua macho ya kiroho (Yoh 3:3; Mdo 26:18).

16.Alituhamisha kutoka gizani akatuingiza nuruni (Yoh 8:12; Mdo 26:18).

17.Alitupumzisha (Matt. 11:28, 29; Ebr. 4:3).

18.Alitupa uzima wa milele (Yoh. 3:16; 5:24; 10:28).

19.Alitufanya watakatifu (Rum. 1:7; 1 Kor. 1:2).

20.Alitutwaa akatufanya watoto wa Mungu (Yoh. 1:12; Efe. 1:5).

21.Alitukomboa kutoka hukumuni (Yoh. 5:24; Rum. 8:1)

22.Alitufanya huru (Yoh. 8:36; Rum. 8:2).

23.Alitubatiza sisi na, au katika Roho Mtakatifu (Matt. 3:11; Mdo. 1:5; Rum. 8:9).

24.Alitupa amani (Rum. 5:1; Efe. 2:14, 17; Yoh. 14:27).

25.Kristo aliye Mwana na Mungu Baba alituchukua kwenye mikono yao kwa ajili ya kututunza salama. (Yoh. 10:28-30).

26.Kristo alifanyika haki yetu (Rum. 1:17; 10:3-4, 6) hekima yetu, ukombozi wetu (1 Kor. 1:30).

27.Alitufanya kiumbe kipya (2 Kor. 5:17; Gal. 6:15).

28.Kristo alikuja ndani yetu kufanya makao (2 Kor. 13:5; Gal. 2:20).

29.Alitukomboa kutoka kwenye kizazi hiki cha sasa kilicho kiovu (Gal. 1:4).

30.Alitufanya warithi wake (Efe. 1:11, 18).

31.Alitufanya kamili katika Kristo (Kol. 2:10).

32.Alitufanyia njia ya kuingia kwenye amani yake hii tuliyomo (Rum. 5:2).

33.Alitukomboa kutoka kwenye laana ya torati (Gal. 3:13).

34.Alitufanya mbegu ya Abrahamu ya kiroho (Gal. 3:29; Rum. 4:16).

35.Alitufanya warithi wa Mungu na warithi pamoja na Kristo (Gal. 3:29; 4:7).

36.Alitufanya wafu kwa kwa maisha ya kale, kwa dhambi na kwa sheria (Rum. 6:2-10; 7:4).

37.Alitubariki kwa baraka zote za rohoni na kimbingu katika Kristo (Efe. 1:3-14).

38.Alitufanya ukuhani wa kifalme, taifa takatifu, watu wa kipekee (I Pet. 2:9).

39.Ametuvuta karibu kwa damu ya Kristo (Efe. 2:13).

Inawezekana mistari mingi iliyoko kwenye orodha hii ikawa na maana inayofanana , lakini kwa kuiweka pamoja inatufanya kuelewa pande nyingi za wokovu wetu.

III. Ni nini Mungu hufanya kwa ajili yetu baada ya kuamini na kwa sababu

                                        tuliamini:

1.  Kristo anatuombea (Ebr. 7:25; Rum. 8:34).

2.  Anatutunza (Yoh. 10:28, Rum. 8:29-35).

3.  Huendelea huko Mbinguni kuifanya kazi nzuri aliyoianza ndani mwetu pale tulipoamini (Filp. 1:6).

4.  Anatuwekea urithi usioharibika, usio na uchafu, ambao haunyauki. (I Pet. 1:4).

5.  Atatufufua siku ya mwisho (Yoh 6:39-40).

6.  Anaturudi kwa faida yetu ili tuwe warithi wa utakatifu wake (Ebr. 12:6-11).

7.  Atatutukuza katika ujio wa pili wa Kristo (Rum. 8:29-30; Filp. 3:21; I Kor. 15:51-57; 1 Yoh. 3:2).

     Katika orodha hii HATUJAWEKA kile Mungu anachotufanyia na anachofanya kupitia sisi kwa sababu ya uaminifu wetu, upendo, kujitoa wakfu na maombi yetu. Kila kitu tulichokiorodhesha hapo juu kinaonyesha sehemu ya Mungu aliyoifanya katika wokovu wetu.

     Sehemu ya Mungu aliyoifanya katika wokovu wetu ni kubwa sana kiasi kwamba mtu mwingine anaweza kudhani mwanadamu hana sehemu kabisa. Lakini kuna upande wa mwanadamu katika wokovu. Mungu amempa mwanadamu UHURU WA UTASHI na Mungu anauheshimu uhuru huo.


Kwa maelezo zaidi kuhusu ACMTC TANZANIA, au jinsi utakavyoweza kujihusisha, wasiliana na Meja Frank & Elina Materu: S.L.P. 7579 Dar es Salaam, Tanzania. Barua pepe: materufrank@yahoo.com